Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewaachia huru aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na aliyekuwa Mkuu wa Fedha na Utawala, Grace Martin, waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni mbili.
Hukumu hiyo iliyovuta watu wengi mahakamani kuja kuisikiliza, ilisomwa jana kwa saa moja na nusu na Hakimu Mfawidhi Ilvin Mgeta ambaye ndiye alikuwa akisikiliza kesi hiyo. Ilianza kusomwa saa 6 kamili mchana.
Katika uamuzi wake, Mgeta alisema anawaachia huru washitakiwa kwa sababu hakuna hata shitaka moja lililothibitishwa dhidi yao na upande wa mashitaka kati ya mashitaka sita yaliyokuwa yakiwakabili.
Baada ya hukumu hiyo, Profesa Mahalu alisema anamshukuru Mungu kwa uamuzi huo na kuongeza kuwa Mungu ametenda kazi kwa kuwapa haki na kwamba baada ya hukumu, anakwenda kumshukuru Mungu kanisani katika Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, Mgeta alisema anashangazwa na upande wa mashitaka kumfikisha mahakamani mshitakiwa Martin ambaye hakuonekana kuhusika kabisa kwa sababu hata nyaraka zilizoletwa mahakamani kama vielelezo, zilisainiwa na Balozi Profesa Mahalu.
Hukumu hiyo ilifafanua kwamba ushahidi wa upande wa utetezi, uliotolewa na Rais mstaafu Benjamin Mkapa, kwamba Mahalu ni mtu muadilifu na mchapakazi na kuwa ameifanyia Serikali mambo mazuri mengi, inaonesha kwamba Serikali ilikuwa inajua kazi yake.
"Shahidi huyo ambaye wakati huo alikuwa kiongozi wa nchini, Rais, alisema kuwa Serikali ilijua kuhusu ununuzi wa jengo hilo la Ubalozi wa Tanzania nchini Italia na ilibariki na pia fedha kuingizwa katika akaunti mbili alifahamu," alisema Hakimu Mgeta na kuongeza:
"Hata hivyo, alisema kuhusu mikataba miwili hakujua hilo, lakini halikuwa tatizo kwa sababu Serikali ilichokuwa ikihitaji ni jengo."
Aidha, alisema Rais wa sasa, Jakaya Kikwete wakati huo alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kwa mujibu wa ushahidi, alitembelea mjini Roma Desemba 2001 na kuona jengo hilo ambapo aliridhika nalo.
Mgeta alisema shitaka la wizi halikuthibitishwa kwa sababu kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa na pande zote, haioneshi kufanyika kwa wizi kwa sababu Serikali ilitoa idhini kwa mshitakiwa Profesa Mahalu kwa kumpa hati au nguvu ya kisheria ya kufanya ununuzi huo kwa niaba ya Serikali.
Kwa mujibu wa hukumu hiyo, Serikali pia iliidhinisha fedha za ununuzi wa jengo hilo kiwango hicho hicho ambacho washitakiwa wanadaiwa kuiba.
Alisema kama Serikali isingeidhinisha mambo hayo kama isingeridhika na hivyo shitaka la kula njama ya kutenda kosa la wizi moja kwa moja linakufa kwa sababu hiyo hiyo.
Hakimu Mgeta alisema anashangazwa na kauli ya baadhi ya mashahidi wa upande wa mashitaka na hasa mpelelezi, aliposema kuwa katika uchunguzi wake, alichogundua katika ununuzi wa jengo hilo taratibu za ununuzi hazikufuatwa.
"Ni nani alipaswa kufuata taratibu, ni watu wa Wizara ya Mambo ya Nje ambao walikuwepo hapa nchini na kutoa maelekezo au ni washitakiwa waliokuwa nchini Italia?" alihoji hakimu huyo.
Alisema ushahidi uliotolewa haukuonesha mazingira kwamba washitakiwa walirudi na kuwashawishi watu wa wizarani kununua jengo hilo.
Hata hivyo, hakimu huyo alisema anaungana na Rais mstaafu Mkapa aliposema katika ushahidi wake kuwa kama ni makosa ya kutumika kwa mikataba miwili ambayo upande wa mashitaka wanadai, ni kosa la Serikali ya Italia na mwenye nyumba haiwahusu washitakiwa.
"Mimi sijui sheria yoyote inayokataza mikataba miwili, washitakiwa wanadaiwa kwa kufanya kosa la jinai la wizi na sio kutumiwa kwa mikataba miwili," alisema.
Washitakiwa hao walidaiwa kufanya malipo katika akaunti mbili tofauti, Mgeta alisema alichoona ni kwamba akaunti zote mbili zilikuwa ni za mwenye nyumba mmoja ikiwa nchini Monaco na nyingine Italia na hakuna uthibitisho wowote kuwa fedha hiyo ilirudi kwa washitakiwa.
Washitakiwa waliofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza mwaka 2007 ambapo kwa mashitaka ya kula njama ya kutenda kosa la wizi na kughushi vocha mbili za ununuzi wa jengo la ubalozi nchini Italia.
Pia walishitakiwa kwa kughushi mikataba miwili ya ununuzi wa jengo hilo na kuidanganya Serikali kuwa walimlipa mnunuzi Euro milioni mmoja wakijua sio kweli.

No comments:
Post a Comment