Thursday, August 23, 2012

JAJI AMTHIBITISHA TJ JACKSON KULEA WATOTO WA MICHAEL JACKSON...

Ni rasmi TJ Jackson sasa atashiriki moja kwa moja katika malezi ya watoto wa Michael Jackson akishirikiana na bibi yao, Katherine Jackson, Jaji wa Mahakama ya Los Angeles ametoa uamuzi huo.
Kama ilivyoripotiwa hapo awali, TJ alipewa jukumu hilo kwa muda katika kuwalea Prince, Paris na Blanket kwa ushirikiano na Katherine, lakini sasa imeamriwa jana kuwa aendelee na jukumu hilo moja kwa moja.
TJ amepokea sapoti kubwa kutoka kwa familia ya Jackson kuweza kubeba majukumu ya malezi, akiwamo Katherine mwenyewe ...na pia watoto wa Michael Jackson. TJ amekuwa kama baba mlezi wa watoto hao kwa miaka kadhaa sasa.
Jaji alimweleza TJ mahakamani kwamba awe na busara katika kubeba jukumu hilo zito ambalo hivi karibuni liliigawa familia ya Jackson vipande ...na kumtaka ahakikishe watoto hawaharibikiwi.
Kama mlezi mwenza, TJ ataendeleza majukumu mengi ya siku hadi siku ikiwamo katika kuwahudumia watoto hao, pamoja na kusimamia vitu vya ndani na ulinzi.

No comments: