Friday, August 24, 2012

CHEKA TARATIBU...

Mwanasheria mmoja wakati akishuka kwenye gari lake aina ya Ferrari ghafla gari jingine likagonga na kunyofoa kabisa mlango wa gari lake. Polisi walipofika eneo la ajali, Mwanasheria akawa analalamika kwa hasira kuhusu uharibifu uliotokea kwenye gari lake analolipenda mno.
Huku akifoka akasema, "Afande! Tazama walichofanya kwenye Ferrari yangu!!"
Afande akajibu, "Nyie wanasheria mnanishangaza, yaani mnathamini mno mali. Unalalamikia haka ka-gari kako badala ya kufikiria mkono wako wa kushoto ambao umekatika katika ajali hii!"
Mwanasheria akapiga kelele kwa sauti akitazama damu ikitiririka katika bega lake la kushoto, "Oooh Mungu wangu! Iko wapi saa yangu ya Rolex?!!" Balaa…

No comments: