Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, leo inatarajiwa kutoa hukumu ya kesi inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na aliyekuwa Mkuu wa Fedha na Utawala katika ubalozi huo, Grace Martin, wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni mbili.
Hukumu hiyo inatarajiwa kusomwa na Hakimu Ilvin Mugeta, anayesikiliza kesi hiyo baada ya kumaliza kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili.
Juni 8, mwaka huu, upande wa utetezi ulifunga ushahidi wao baada ya mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo, Martin kumaliza kujitetea.
Miongoni mwa mashahidi waliopanda kizimbani kumtetea ni Profesa Mahalu ni Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ambaye alidai mahakamani kuwa anashangaa kufikishwa washitakiwa hao mahakamani kwa sababu anachojua yeye Serikali ilibariki ununuzi wa jengo hilo.
Washtakiwa walipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza mwaka 2007 wakikabiliwa na mashitaka sita, ambayo ni kula njama kutenda kosa la wizi na kughushi vocha ya malipo ya ununuzi wa jengo.
Mengine ni kughushi mikataba miwili ya ununuzi wa jengo hilo kwa ajili ya kuidanganya Serikali, kutumia risiti ya ununuzi wa jengo hilo kuidanganya ili waioneshe kwa Serikali kuwa walimlipa muuzaji euro milioni moja wakati si kweli na kuisababishia Serikali hasara ya kiasi hicho cha fedha za kigeni.
Kwa mujibu wa ushahidi wa washitakiwa hao wakati wakijitetea, walidai kuwa walinunua jengo hilo la ubalozi kwa ridhaa ya Serikali chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wizara ambayo ilikuwa ikiongozwa na waziri wa wakati huo ambaye sasa ni Rais, Rais Jakaya Kikwete.

No comments:
Post a Comment