Hoskins mwenye miaka 69 ametoa taarifa hiyo jana, akidai kuwa amegundulika kuwa na maradhi hayo. Pia amewashukuru mashabiki wake kwa msaada wao, akisema alikuwa na wakati mzuri sana kipindi chote cha uigizaji wake.
Bila masihara, kipindi chake cha uingizaji ameweza kucheza filamu zisizopungua 80, na mchango wake katika filamu za Uingereza kupitia "The Long Good Friday" na "Mona Lisa" ulimuwezesha kupata Tuzo za Cannes, Tuzo za Golden Globe kwa Mwigizaji Bora, Tuzo kadhaa za BAFTA na kuchaguliwa kushiriki kwenye Academy Award.
Kisha tena, Hoskins alicheza katika tukio la moja kwa moja mwaka 1993 kwenye "Super Mario Bros".

No comments:
Post a Comment