Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi alisema Fatuma alikutwa amekufa baada ya kujinyonga juzi saa 11.00 jioni kwake Chanika.
Mbali na kumdai baba mkwe wake, Fatuma pia katika ujumbe huo alisema; “nimechanganyikiwa mwanangu kazi hana, sitaki wanangu waende kiumeni (kwa ndugu wa baba yao), waangalieni kikeni tu (kwa ndugu wa mama yao).”
“Baba mdogo uza nyumba (watoto) wapate pa kukaa, bonge kachukua fedha nyingi sana Sh 1,000,000 peke yake… najuta kuuza nyumba ya Lumo ningejua nisingekubali kuuza,” ujumbe wa Fatuma ulieleza.
Kwa mujibu wa Kamanda Minangi, mwili wa marehemu Fatuma umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili huku polisi wakiendelea na upelelezi zaidi.

No comments:
Post a Comment