Ndege ya abiria imeanguka katika eneo lenye msongamano wa makazi ya watu katika mji mkubwa wa Nigeria jana, kuua watu wote 153 na kujeruhi vibaya wengine waliokuwa ardhini katika ajali mbaya zaidi kutokea nchini humo katika kipindi cha karibu karne mbili.
Chanzo cha ajali hiyo ya ndege ya Dana hakijafahamika hadi jana usiku, wakati askari wa vikosi vya zimamoto na polisis wakihangaika kuzima moto uliozingira eneo ilipoanguka ndege hiyo aina ya Boeing MD83.
Mamlaka zimeshindwa kudhibiti umati wa maelfu ya wakazi waliokusanyika pamoja kushuhudia ajali hiyo, baadhi wakisimama juu ya bawa la ndege hiyo lililokatika.
Harold Demuren, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga, alisema abiria wote walikuwamo wamekufa katika ajali hiyo. Serikali ya Jiji la Lagos ilisema katika taarifa yake kwamba watu 153 walikuwa kwenye ndege hiyo wakisafiri kutoka mji ulio katikati ya Nigeria wa Abuja kuelekea Lagos, mji ulio kusini-magharibi mwa nchi hiyo.
Maofisa wa uokoaji wanahofia kuna wengine zaidi wamekufa ama kujeruhiwa ardhini, lakini hakuna idadi kamili iliyopatikana ya majeruhi.
Askari wa zimamoto na wananchi wa kawaida walionekana wakibebea mwili wa mwanaume mmoja kutoka kwenye jengo moja huku kuta zake zilikuwa zikiendelea kuwaka moto ulioenea mpaka kwenye paa lake zaidi ya saa moja tangu kuanguka kwa ndege hiyo.
Rais Goodluck Jonathan baadaye alitangaza siku tatu za maombolezo ya taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu.
"Tuombe Mwenyezi Mungu azijaze uvumilivu na utulivu familia za waathirika wote wa ajali ya ndege kutokana na kupoteza wapendwa wao," taarifa kutoka ofisi ya Rais ilisema.
No comments:
Post a Comment