Tuesday, June 5, 2012

MWIMBAJI NAS 'ACHEMKA' TAREHE YA KUZALIWA BINTI YAKE...



Mwimbaji Nas ana kila sababu ya kufurahi kwamba binti yake ana hisia nzuri ya vichekesho, sababu imeelezwa ameipenda mno video ya muziki wa wimbo alioumbiwa na baba yake kama zawadi ya siku yake ya kuzaliwa, japo tarehe yake ya kuzaliwa iliandikwa kimakosa.
Video ya binti huyo imeanza kwa kutokea jina la Destiny Jones na tarehe yake ya kuzaliwa "Septemba 14", lakini kiusahihi hiyo ni tarehe ya kuzaliwa Nas. Video hiyo imetolewa maalumu kukumbukia siku ya kuzaliwa Destiny ambayo ni Juni 15. 
Nas mwenyewe amefafanua kutia mtandao wa Tweeter kwamba imetokana na aliyehariri video hiyo kuchanganya tarehe hizo.
Vyanzo vya habari vilivyo karibu na Destiny vimeeleza jinsi binti huyo alivyoikubali na kuipenda mno video hiyo. Lakini kwakuwa Nas anaikumbuka vizuri tarehe ya kuzaliwa binti yake, hakuna tatizo katika hili.

No comments: