Lulu akitoka mahakamani akiwa chini ya ulinzi mkali wa Askari Magereza leo.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya mauaji inayomkabili muigizaji wa filamu Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, hadi Juni 18 mwaka huu itakapotajwa tena.
Wakili wa Serikali, Peter Sekwao aliieleza mahakama hiyo kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kuiomba mahakama ipange tarehe nyingine.
Lulu anakabiliwa na mashitaka ya mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba ambapo anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 7, mwaka huu katika eneo la Sinza Vatican jijini Dar es Salaam. Hakimu Agustina Mmbando aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 18 mwaka huu itakapotajwa tena mahakamani hapo.

Katika kesi hiyo, Lulu anatetewa na mawakili, Peter Kibatala, Fulgence Masawe, Kennedy Fungamtama na Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG) Joaquine De- Melo aliyetambulishwa kama mtazamaji.
Aidha uamuzi wa ombi la kuchunguza umri wa Lulu lililowasilishwa katika Mahakama kuu utatolewa Juni 16 mwaka huu na Jaji Fauz Twaib.
Mawakili wanne wanaomtetea Lulu waliwasilisha ombi la kuchunguza umri wa Lulu na kuomba kesi hiyo ihamishwe Mahakama ya Watoto kwa kuwa Lulu ana miaka chini ya 18.
Mawakili wanne wanaomtetea Lulu waliwasilisha ombi la kuchunguza umri wa Lulu na kuomba kesi hiyo ihamishwe Mahakama ya Watoto kwa kuwa Lulu ana miaka chini ya 18.
Utata wa umri wa Lulu unatokana na hati ya mashitaka kuandika kuwa ana umri wa miaka 18 na yeye kukana kwa madai kuwa ana umri wa miaka 17.

No comments:
Post a Comment