Sunday, June 24, 2012

CHEKA TARATIBU...

Mwalimu alikuwa akifundisha wanafunzi kuhusu mzunguko wa damu mwilini. Akijitahidi kuwaelewesha vizuri akatoa mfano, "Sasa wanafunzi. Kama nikisimama kwa kutumia kichwa, damu kama unavyojua itakuja kichwani na usoni nitakuwa mwekundu kabisa."
Wanafunzi wakajibu, "Ndioooooo."
Mwalimu akaendelea, "Sasa kwanini hivi nilivyosimama kawaida damu haikimbilii miguuni?"
Sauti ndogo kutoka nyuma ya darasa ikasikika, "Sababu miguu yako haiko tupu, INA KITU NDANI!" Kasheshe...

No comments: