Monday, May 7, 2012

WAOMBA KESI YA LULU IHAMIE MAHAKAMA YA WATOTO...


Msanii Lulu akiingia mahakamani leo huku akiwa chini ya ulinzi mkali wa askari Magereza.
Wakati msanii wa filamu, Elizabeth Michael 'Lulu' akipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo, Wakili anayemtetea msanii huyo, Kenedy Fungamtama ameiomba Mahakama hiyo ihamishie kesi hiyo ya madai ya kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba, katika Mahakama ya Watoto kwa kuwa mteja wake ana umri chini ya miaka 18.
Upande wa mashitaka ulieleza kushangazwa na ombi hilo kwa madai kwamba mahakama hiyo ambako kesi inatajwa haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo ya mauaji.
Wakili wa Serikali katika kesi hiyo, Elizabeth Kaganda alidai kwamba kesi hiyo ipo katika hatua ya upelelezi ambao haujakamilika na kwamba miongoni mwa vitu wanavyochunguza ni pamoja na umri wa mshitakiwa huyo.
Katika kesi hiyo iliyotajwa jana mbele ya Hakimu Agustina Mmbando, wakili huyo aliomba mahakama imuone Lulu kuwa hajafikisha umri wa miaka 18.

No comments: