Tuesday, May 8, 2012

KIJANA AJIUA KUMFUATA MAMA YAKE KUZIMU...

KUSHOTO: Deborah Collier (juu) na mwanae Liam Collier. KULIA: Msitu ambamo Liam alijinyonga na kufariki.
Kijana wa miaka 15 anaaminika kujiua baada ya mama yake kufa kwa saratani.
Kijana huyo aliyetajwa kwa jina la Liam Collier alikutwa kwenye kichaka cha miti karibu na nyumbani kwake na alithibitishwa kufariki eneo la tukio.
Anaaminika alikufa kwa kujinyonga na uchunguzi wa mwili wake ulitarajiwa kufanyika baada ya muda mfupi.
Mama yake Deborah Collier aliyekuwa na miaka 35, alifariki ghafla Februari 24 baada ya kupambana na ugonjwa wa saratani.
Marafiki wameeleza kijana alikatishwa tamaa baada ya kufariki mama yake na aliwaambia 'nataka kuungana na mama yangu.'
Jirani anayeishi kwenye mtaa aliokuwa akiishi Liam alisema kuwa binti yake alikuwa rafiki wa kijana huyo na alisikia kutoka kwa mwenzao kwamba Liam amejinyonga.
Alisema: "Nimekufa ganzi. Rafiki zake walimshusha mara ya kwanza bila kujua kama angejaribu tena kujinyonga."Alisema kifo cha Liam kimechangiwa na kilichomtokea mama yake.
Alisema: "Nimekuwa nikiambiwa allikuwa akisema 'Nataka kuungana na mama yangu'. Naona ndio sababu pekee ya yeye kuchukua uamuzi huo.
"Mama yak alidhoofika kwa takribani miaka miwili. Kisha wakafikia mwisho wao."
Marafiki walifikiria kukuta mwili wake kwenye miti mjini Barnsley Jumatatu iliyopita jioni na kujaribu kumshusha chini.
Msemaji mmoja kwa niaba ya familia ya Liam amethibitisha kuwa baba yake, Alan tayari amepoteza mke wake na 'amechanganyikiwa sana.' Rambirambi kadhaa zimetumwa kwa njia ya baruapepe kufuatia msiba wa kijana huyo.
Msemaji wa Polisi wa South Yorkshire alisema: "Polisi wa South Yorkshire waliitwa saa 2:30 usiku baada ya tukio kwenye eneo la miti mjini Barnsley.
"Huduma za dharura ziliwasili eneo la tukio na muda mfupi baadaye kijana huyo akatangazwa kuwa amefariki."

No comments: