Tumeweka video hii katika kukumbushana usalama barabarani ambapo matukio kama haya yanafanyika hapa Tanzania.
Video inaonesha tukio la kushitusha ambapo mwanaume mmoja ambaye hakufahamika aligongwa na gari kwenye moja ya barabara kuu za nchini Urusi hivi karibuni.
Mwanaume huyo alishuka na kuzagaa kando ya gari lake kwenye barabara kuu yenye njia tatu, ndipo ajali ikatokea.
Anaonekana akitembea kando ya gari lake ya kijivu akielekea nyuma kwenye buti lililo wazi. Inasemekana alisimama kwa dharura, bila kuweka alama yoyote wala kuwasha indiketa za tahadhari.
No comments:
Post a Comment