Tuesday, May 22, 2012

USHER AMWAGA CHOZI KORTINI...


Mwimbaji Usher Raymond amemwaga machozi kortini baada ya wakili wa aliyekuwa mkewe kumpiga kijembe kwamba anaendekeza kujirusha tu badala ya kutunza watoto wake.
Usher alisimama kizimbani kwa masaa kadhaa leo kusikiliza kesi inayomkabili dhidi ya mkewe wa zamani, Tameka Foster na wakati wa maswali, Wakili wa Tameka alionesha picha za mwimbaji huyo akijirusha huko Ulaya mwezi Februari, mwaka huu. 
Mwimbaji huyo anapigania kuonesha kwamba yuko karibu na watoto wake lakini wakili wa Tameka anajaribu kuthibitisha kuwa Usher anaona sawa kwenda klabu za usiku badala ya kuwa baba bora.
Pia Usher anatuhumiwa kwa matumizi ya dawa za kulevya. Mwimbaji huyo alikiri kuvuta bangi siku zilizopita, lakini kuhusu kuhamia katika dawa za kulevya wakili wake alikanusha vikali.
Usher alisisitiza hakuwahi kutumia dawa za kulevya mbele ya watoto wake, tuhuma zilizotolewa na Tameka mwanzoni mwa mashitaka yao ya kumiliki watoto.
Kesi hiyo inaendelea.

No comments: