Tuesday, May 22, 2012

MPENZI WA ZAMANI WA WHITNEY ATIMULIWA TUZO ZA BILLIBOARD...

Mwanamuziki Ray J akiingia kwenye Tuzo za Musiki za Billiboard juzi usiku.
Aliyewahi kuwa mpenzi wa mwimbaji Whitney Houston, Ray J usiku wa juzi alikaribia kutolewa nje wakati wa Tuzo za Muziki za Billiboard baada ya wanafamilia wa Whitney kuwaamuru walinzi kumuondoa karibu yao, imefahamika.
Wifi wa Whitney, Pat Houston alifura kwa hasira sababu yeye, Bobbi Kristina na wanafamilia wengine walikuwa wameketi jirani na Ray J, mtu ambaye wanaamini amechangia kiasi kikubwa kumharibu Whitney. Dakika chache kabla ya kwenda kupokea tuzo ya Whitney, Pat aliwaamuru walinzi wake kumuhamisha Ray J kwenye kiti chake, lakini mwanaume huyo aligoma kuhama.
Vyanzo vya habari vimesema, walinzi wa Pat waliungana na walinzi wa hoteli sambamba na askari wenye sare kumhamisha kinguvu Ray J.
Kabla ya kumsukuma, ilikaribia kuibua vurugu ndipo walinzi wakamtahadharisha Pat kuwa kitendo hicho kitatengeneza stori kwani ilikaribia kunaswa kwenye video muda mfupi kabla ya Whitney kutuzwa.
Baadaye Pat akalazimika kunywea na Ray J kurejea kwenye kiti chake.
Kwa upande wake, Ray J amelalamika kwa marafiki zake kwamba, "Pat amefuta nafasi ya kipekee kwake kumtunuku mwanamke aliyempenda sana."

No comments: