MGM Grand ya mjini Las Vegas imeanzisha uchunguzi wa ndani kuhusu picha za video zilizomnasa binti wa Whitney Houston mwenye umri mdogo, Bobbi Kristina akicheza kamari kwenye moja ya casino zake mwishoni mwa wiki.
Katika video hiyo anaonekana Bobbi mwenye miaka 19 akicheza kamari Jumamosi usiku akiwa na rafiki yake wa kiume mwenye miaka 22. Bobbi alikuwa mjini humo kuhudhuria Tuzo za Muziki za Billiboard zilizofanyika Jumapili.
Mwakilishi wa MGM kwa sasa anafuatilia tukio hilo.
Tume ya Michezo ya Kubahatisha ya Nevada nayo pia imeanzisha uchunguzi binafsi kuhusiana na picha hizo za video.
Kamari kwa watu walio na umri mdogo ni marufuku mjini Nevada, na adhabu yake inafikia hadi kifungo cha miezi sita jela au faini ya Dola za Kimarekani 1,000. MGM Grand inaweza kukabiliwa na faini hiyo.

No comments:
Post a Comment