Tuesday, May 29, 2012

UCHUNGUZI WA KIFO CHA BONDIA TAPIA WAANZA RASMI...


Mamlaka leo zilitarajiwa kufanya uchunguzi kuhusu Johnny Tapia, ikiwa siku mbili baada ya bondia huyo kukutwa amekufa nyumbani kwake, imefahamika.
Vyanzo vya kisheria vimeeleza kuwa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa New Mexico ilipanga kufanya uchunguzi wa kifo hicho ikiwamo matumizi ya dawa za kulevya kujua sababu hasa za kifo chake.
Kama ilivyoripotiwa awali, mwili wa bingwa huyo mara tano wa dunia ulikutwa na ndugu zake Jumapili iliyopita jioni. Polisi walisema hakuna aliyekamatwa kuhusiana na kifo hicho.
Tapia amefariki akiwa na umri wa miaka 45.

No comments: