Tuesday, May 29, 2012

KUTOKA MAGAZETINI LEO...

              HABARI ZILIZOSISIMUA             

KANISA LACHOMWA ZANZIBAR
Kanisa Katoliki Parokia ya Mpendae limechomwa moto jana na watu wasiojulikana ikiwa ni mfululizo wa matukio ya kuchomwa makanisa Visiwani Zanzibar baada ya lile la Assemblies of God wiki iliyopita.
Kiongozi wa Kanisa hilo, Ambaros Mkenda, alidai kwamba Kanisa hilo lilichomwa moto na kusababisha uharibifu mkubwa.

Alidai Kanisa hilo lilichomwa moto jana saa 8.30 mchana na watu wanaohisiwa kuwa wafuasi wa Jumuiya ya Kiislamu ya Uamsho, waliokuwa wakitoka katika Mahakama ya Mwanakwerekwe kusikiliza kesi ya wenzao waliokamatwa juzi. Habari zaidi pata nakala yako sasa! 
-HABARILEO Mei 29.


AMUUA BABA, AMJERUHI MAMA YAKE
Polisi wa Mpanda mkoani Katavi inamshikilia Leocadus Maembe (41), wa kijiji cha Kasinde, tarafa ya Kabungu kwa madai ya kumwua baba yake mzazi, kwa mapanga kwa kinachodaiwa ni ugomvi wa shamba.
Pia inadaiwa kuwa mshitakiwa huyo alimshambulia na kumjeruhi pia mama yake mzazi, Olievetha Mwaisanga aliyeingilia ugomvi huo ili kuwasuluhisha baba na mwanawe.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Joseph Myovela alisema jana kuwa mauaji hayo ya Anthony Costantino ‘Kajalanga’ (69), yalifanyika Mei 19 saa 2 usiku jirani na nyumba ya marehemu huyo kijijini hapo. Habari zaidi pata nakala yako sasa!
-HABARILEO Mei 29.

No comments: