Mwimbaji mkongwe wa kundi la Bee Gees, Robin Gibb amefariki dunia jana baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na maradhi ya saratani. Amefariki akiwa na umri wa miaka 62.
Msemaji wake ametoa taarifa inayosomeka, "Familia ya Robin Gibb wa Bee Gees, inatangaza kwa huzuni kubwa kwamba Robin amefariki leo kutokana na maradhi ya saratani yaliyomsumbua kwa muda mrefu na upasuaji wa utumbo mkubwa. Familia inaomba utulivu katika kipindi hiki kigumu."
Gibb alichunguzwa miaka miwili iliyopita na kugundulika kuwa na saratani ya ini. Alilazwa hospitali mara kadhaa katika miaka michache iliyopita, na mara ya mwisho ilikuwa mwezi uliopita.
Gibb alipata tuzo za Hall of Fame kama Mwandishi Bora wa Nyimbo mwaka 1994 na bendi yake ikanyakua tuzo hizo kama bendi bora ya miondoko ya Rock and Roll miaka mitatu baadaye.
Albamu ya 'Saturday Night Fever' ilitikisa mno sokoni kwa kuuza nakala nyingi kabla ya Michael Jackson kuteka soko kwa albamu yake ya 'Thriller'.

No comments:
Post a Comment