Monday, May 28, 2012

MACHINJIONI YAANZA TENA KUSAKA ROHO ZA WATU...


Ajali mbaya imetokea mchana huu kwenye makutano ya Barabara za Chang'ombe na Mandela eneo maarufu kwa ajali la 'Machinjioni' ambapo daladala aina ya Mitsubishi  Rosa lenye namba za usajili T 987 BDH linalofanya safari kati ya Mwenge na Temeke na gari dogo aina ya Suzuki Grand Vitara mali ya Legal Sector Reform Program lenye namba T 305 AEN. Cha ajabu kwenye makutano hayo kuna taa za kuongozea magari ambazo zilifanya kazi kwa siku mbili tu na kisha zikazimwa. Baada ya hapo kila mara zimekuwa zikitokea ajali mfululizo kutokana na kila dereva kujiona ana haki! Kituko ni kwamba baada ya ajali kutokea ndipo akaja askari wa usalama barabarani na kuanza kazi ya kuongoza magari. Uzembe huu mpaka lini?
Mmoja wa mashuhuda akilitazama gari dogo lililoharibiwa vibaya katika ajali hiyo. (Picha zote na mpigapicha maalumu).

No comments: