Monday, May 28, 2012

JUSTIN BIEBER ASAKWA KWA KUMDUNDA PAPARAZZI...


Mwimbaji Justin Bieber anasakwa kwa tuhuma za kumshushia kisago mpigapicha aliyekuwa akijaribu kupata picha ya Bieber wakati akiwa kwenye Duka la The Commons, mjini Calabasas anakoishi.
Imeelezwa baada ya kurushiana maneno ndipo Justin akamvaa mpigapicha huyo na kuanza kumshushia masumbwi kabla ya kutokomea na mpenzi wake kusikojulikana.
Mpigapicha huyo alipiga simu polisi ambao hata hivyo walifika wakati Bieber na mpenzi wake, Selena Gomez wakiwa wameshakimbia eneo la tukio.
Mpigapicha huyo alikuwa akilalamika maumivu sehemu mbalimbali mwilini na ikalazimu kuchukuliwa kwa gari la wagonjwa kupelekwa hospitali kwa matibabu. Alitibiwa na muda mfupi baadaye kuruhusiwa.
Wakati polisi wanachunguza tukio hilo, imeelezwa na baadhi ya mashuhuda kwamba wanasheria walimfuata mpigapicha na kushawishi kwamba anaweza kutengeneza pesa nyingi kutokana na tukio hilo na kwamba wakamtaka aripoti polisi na kuita gari la wagonjwa.
Mashuhuda waliongeza kwamba mpigapicha huyo alikuwa amelizuia gari la Bieber wakati akijaribu kuondoka. Mwimbaji huyo akashuka kwenye gari na kumtaka mpigapicha huyo kupisha njia lakini akagoma na mzozo kuanza.

No comments: