Monday, May 28, 2012

BONDIA JOHNNY TAPIA AFARIKI DUNIA...


Bondia Johnny Tapia ameripotiwa kufariki dunia jana.
Wanafamilia wamesema Polisi wa Albuquerque waliitwa nyumbani kwa Tapia majira ya saa 1:45 usiku baada ya wanafamilia kugundua mwili wake.
Polisi wamesema kifo chake ni cha kawaida, lakini sababu rasmi ya kifo chake bado haijajulikana.
Tapia, ni bingwa wa dunia mara tano. Mke wake ameshitushwa na janga hilo. Baba wa Tapia aliuawa wakati mama yake akiwa na ujauzito wake. Na Tapia alipokuwa na miaka nane, mama yake alitekwa nyara, kubakwa na kunyongwa.
Tapia alilazwa hospitali mwaka 2007 akiwa katika hali mbaya kutokana na kutumia dozi kubwa ya cocaine. Siku moja baada ya kulazwa, shemeji yake na mtoto wa dada yake walikufa kwenye ajali ya gari wakiwa njiani kwenda kumtembelea hospitalini.

No comments: