Manchester City wametwaa ubingwa wao wa kwanza wa Ligi Kuu ya England kwa mara ya kwanza tangu walipofanikiwa kufanya hivyo miaka 44 iliyopita. Kama haitoshi, Man City wametwaa ubingwa msimu huu kwa kuwatambia mahasimu, Manchester United baada ya kuwafunga katika mechi zote mbili walizokutana nao (Ya kwanza kwenye Uwanja wa Old Trafford wakishinda mabao 6-1 na ya pili Uwanja wa Ettihad wakishinda bao 1-0). Pia, wachezaji walioibeba Man City mwanzoni mwa msimu, Sergio Kun Aguero na Edin Dzeko kwa kufunga mabao lukuki ndio haohao walioibebesha ubingwa timu yao kwa kufunga mabao muhimu jana (Dzeko akifunga bao la kusawazisha na Aguero akifunga la ushindi). Mabao yote muhimu yalifungwa baada ya dakika 90. Rekodi mpya katika ligi ya England ni kwamba hii imekuwa mara ya kwanza katika historia ya ligi hiyo bingwa kuamuliwa kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa. Mchezaji Samir Nasri ametimiza ndoto yake ya kutwaa vikombe kama alivyobainisha wakati wa kuondoka kwake Arsenal. La mwisho kabisa kukushirikisha ni kwamba licha ya mafanikio ya Manchester United, ukweli unabaki kwamba Manchester City ndio klabu kubwa maarufu yenye mashabiki lukuki katika jiji la Manchester.

No comments:
Post a Comment