Monday, May 14, 2012

DEFOE ASHUSHA BEI YA JUMBA LAKE ILI LIPATE KUNUNULIWA...

Mwanasoka wa England, Jermain Defoe amepunguza bei ya jumba lake lililoko Hertfordshire kwa Pauni za Uingereza 575,000 katika juhudi zake kuona linapata mnunuzi haraka.
Jumba hilo lenye vyumba sita cya kulala lililojengwa kwa ajili ya mshambuliaji huyo wa klabu ya Tottenham Hotspurs mwaka 2007 linajumuisha chumba cha michezo mbalimbali, ukumbi mdogo wa sinema na vyumba maalumu vya kubadilishia nguo.
Rafiki yake wa kike wakati huo pia alitaka lijengwe jiko kwa thamani ya Pauni za Uingereza 200,000.
Kitegauchumi hicho, ambacho mwaka jana kilithaminiwa Pauni za Uingereza 3,750,000 lakini sasa baada ya punguzo hilo linaweza kununulika kwa Pauni za Uingereza 3, 175,000, pia lina gym yenye bafu la kuogea na sauna, chumba cha chakula, bustani na geti kubwa lililozungukwa na uzio mrefu.
Jumba hilo lipo kwenye kijiji cha Cuffley, ambako sasa pamebatizwa jina la 'Mstari wa Mamilionea' kutokana na kujaa makazi ya wasanii maarufu eneo hilo.
Watu maarufu ambao ni majirani wa Defoe ni pamoja na wachezaji wenzake wa Tottenham, Ledley King na David Bentley, Sir Terry Leahy na mtangazaji wa televisheni Myleene Klass pia anaishi jirani na hapo.
Defoe mwenye miaka 29, ambaye amemchumbia mshindi wa X Factor, Alexandra Burke, amepanga kuhamia kwenye jumba lake lililoko Chigwell, Essex, hivi karibuni.
Jumba hilo linalouzwa lina eneo la ukubwa wa futi za mraba 7,000 ambalo limejengwa kwa ustadi wa hali ya juu huku likiwekewa geti linalofunguliwa kwa rimoti na uzio mrefu kuzunguka eneo hilo.

No comments: