Dada mmoja akiwa amechanganyikiwa baada ya kupata taarifa kwamba baba yake kalazwa hospitali kaenda kwenye duka la dawa kununua dawa maeneo ya Keko Magurumbasi. Dada huyo kwa biashara ya kuuza dawa za kukuza makalio, kapigiwa simu kwamba apeleke dawa za maumivu kwa kuwa hazikuwapo hospitalini hapo. Baada ya kupatiwa dawa hizo, akazitupia tu kwenye pochi yake na kutimua mbio. Kufika hospitali kwa haraka akatoa vidonge bila kuangalia na kumpatia baba yake ambaye kwa hali aliyokuwano akabwia fasta na kujilaza kitandani. Wakati dada huyo akitoa simu kwa mshangao akaona dawa za maumivu ndani ya pochi. Toba, kumbe kampatia baba yake dawa za kukuza makalio! Unaambiwa dada akatimua mbio kwenda nje akilia huku manesi wakibaki wanashangaa...

No comments:
Post a Comment