Meneja wa Fedha aliyemsababishia mwanafunzi majeraha makubwa na kumwacha akiwa mahututi baada ya kumkata kwa glasi ya mvinyo shingoni, ameachiwa huru baada ya Jaji kumtaja kuwa ni 'mwanamke mtulivu'.
Mrembo Claire Stephens mwenye miaka 23, alimshambulia Rachel Spikula baada ya wawili hao kukongana jukwaani wakicheza muziki ukumbi wa Club 49, West End jijini London.
Raia wa Marekani alikimbizwa hospitali kwa kutumia gari la wagonjwa baada ya kupata majeraha kadhaa kwenye mshipa mkubwa wa damu katika ugomvi mapema Juni 11, 2011.
Mwendesha Mashitaka Gavin Ludlow-Thompson alisema muathirika angeweza kuwa hatarini kama asingetibiwa haraka sana.
"Mapendekezo yametolewa kwamba kama gari la wagonjwa lisingekuwapo na huduma ya kwanza isingepatikana haraka, basi muathirika huyo angepoteza maisha yake," alisema.
Lakini Jaji Nicholas Loraine-Smith alimwepusha Claire na kifungu cha kifungo baada ya kusikia ni "mwanamke kijana mtulivu na mchapakazi."
Akitoa hukumu ya kifungo cha miezi 10 jela, kufungiwa kwa miaka miwili, alisema: "Hakuna cha kushawishi kwamba hukuwahi kuhusika kwenye ghasia hapo kabla - zaidi inaonekana kinyume kabisa, hii hukuwa jinsi ulivyo.
"Lakini usiku huo ukabadili kabisa maisha ya mwanamke kijana. Majeraha uliyomsababishia yanaweza kuwa athari itakayodumu kwa kipindi kirefu.
"Imeshabadili kabisa maisha yake na kuleta madhara makubwa kwa familia yake, na hakuna hukumu nitakayotoa itakayobadili hayo."
Claire, Meneja wa Fedha katika kampuni moja ya vitegauchumi na mipango, alitoka na rafiki zake kwenda Club 49 iliyoko mtaa wa Greek, mjini Soho, ambako yeye na Rachel walipambana baada ya kugongana kwenye jukwaa la kuchezea.
Katika harakati za kumtoa Rachel, Claire akampiga kwa glasi mbaya wake huyo shingoni na kumkata kwa ncha ya glasi hiyo.
Ludlow-Thompson alisema kwamba alikimbizwa hospitali na kuruhusiwa baada ya masaa 18, kabla ya kurejeshwa tena hospitali kufuatia hali yake kuwa mbaya wiki chache baadaye.
Vipimo vimebainisha jeraha limesababisha 'matatizo ya shinikizo la damu' na madaktari walilazimika kufanya upasuaji kuziba mshipa huo wa damu.
"Sasa ana mishipa mitatu inayopeleka damu kwenye ubongo badala ya minne." alisema mwendesha mashitaka.
"Sasa anaugua tatizo la kupoteza umakini na analazimika kuendelea na matibabu kila mwaka."
Kufuatia shambulio hilo, Claire aliondoka ukumbini hapo kabla ya kukiri kwa rafiki wa baba yake, ambaye alimwambia akajisalimishe polisi.
Katika utetezi, Wakili Gary Pons alisema tukio zima limetawaliwa na 'madhara ya kisaikolojia' kwa mteja wake.
Alisema: "Kwa sasa ni mkimya sana na amejitenga na wala hatoki nje, anapofanya hivyo basi hanywi na mara kwa mara hutokwa machozi."
Claire anayetokea Harlow, mjini Essex amekiri kuvunja sheria kwa kujeruhi.
Amehukumiwa kutotoka kati ya Saa 3 usiku hadi Saa 12 asubuhi, akitakiwa kufanya kazi za kujitolea kwa masaa 240, na kutakiwa kulipa fidia ya Pauni za Kiingereza 9,100 pamoja na Pauni za Kiingereza 500 za gharama za kesi.

No comments:
Post a Comment