Sunday, May 20, 2012

CHEKA TARATIBU...


Mvutaji dawa za kulevya mmoja maarufu kama 'teja' kajituliza zake maeneo ya Posta ya Zamani akipunga upepo wa Bahari ya Hindi.
Kutokana na kuchoka maisha ya Bongo kaamua kuzamia zake meli. Giza lilipoingia akaelekea bandarini zinakoegeshwa meli na kujificha ndani ya meli moja bila kuonekana na yeyote. Baada ya masaa kadhaa meli ile ikaanza kuondoka huku yule teja akijipongeza kwamba tayari kaicha Bongo. Kwa bahati mbaya, nahodha wa meli ile akapewa amri kusitisha safari na kutii amri hiyo. Siku kadhaa kupita huku yule teja akiamini tayari meli imefika mbali, akaamua kutoka na kuogelea mida ya usiku hadi ufukweni. Mtu wa kwanza kukutana naye alikuwa mweusi kama yeye. Yule mtu bila kusita akamsalimia teja, "Habari yako kaka? Vipi mbona uko hapa peke yako, kuna tatizo?" Teja akashtuka na kujibu, "He, wewe lazima umetoka Tanzania. Unaongea Kiswahili kizuri kabisa!" Jamaa akajibu, "Nimezaliwa hapa hapa Tanzania." Kusikia hivyo Teja akabaki mdomo wazi na alipogeuza kichwa akaona daladala la Mwananyamala-Kivukoni likikatisha! Hapo akaishiwa nguvu kabisa, kumbe alikuwa Feri!

No comments: