Sunday, May 20, 2012

AMWAGIWA TINDIKALI BAADA YA KUMKATALIA MWANAUME NDOA...


Msichana wa Afghanistan amesimulia tukio lake la kutisha ambalo limemwachia hofu kubwa maishani baada ya mwanaume aliyekataa kuolewa naye kumshambulia kwa tindikali.
Mumtaz mwenye miaka 18, amekuwa muathirikawa tukio ambalo mwanaume aliyeamua kama binti huyo hataolewa naye, basi anahakikisha hatatokea mwanaume yeyote kumuoa.
Mumtaz anasema: "Najisikia vibaya, sipendi tena kujiangalia sura yangu kwenye kioo."
Mwanaume huyo alimtaka wafunge naye ndoa, lakini familia ya Mumtaz ilikataa maombi yake hayo.
Kisha, alisema usiku mmoja wanaume kadhaa walifika nyumbani kwao na kuishambulia familia yake.
Mwishowe wanaume wawili wakamshika, wakamuinua kichwa na kumpa nafasi mwanaume huyo aliyetaka kumuoa ammiminie tindikali kuzunguka uso wake.
"Nililazwa hospitali kwa siku 10 mjini Kunduz, na baadaye wakanileta mjini Kabul," amesema Mumtaz. "Sehemu kubwa ya mwili wangu iliungua. Daktari aliponiwekea dawa nilihisi kama nimetoswa kwenye moto."
Wanaume wachache wamekamatwa lakini hayumo yule aliyehusika na kubadilisha milele sura ya Mumtaz.
Hii ilikuwa mara ya kwanza kuruhusu kuonesha sura yake hadharani na kusimulia mkasa wake kwenye televisheni, kwa kiasi fulani anahofia maisha yake.
Mumtaz kwa sasa anaishi kwenye makazi maalumu ya wanawake walionyanyaswa kijinsia ambapo kwa wapo wanawake 16, baadhi wakiwa na watoto wadogo.
"Makazi haya yametusaidia mno. Kama wasingekuwapo kunisaidia, ningekuwa nimeshakufa mpaka sasa. Maisha yangu yalikuwa kwenye hatari kubwa," alisema Mumtaz.
Mumtaza anajifunza kusoma na kuandika kwa mara ya kwanza na anaamini atapata matibabu zaidi nchini India.
Rais wa Afghanistan, Hamid Karzai ametia saini muswada wa sheria yenye lengo la kumaliza uonevu dhidi ya wanawake nchini humo.
Wanaharakati wa haki za wanawake wamesema sheria hiyo ni nzuri lakini msukumo kwa sheria hiyo ni legelege.

No comments: