Jamaa mmoja karejea zake nyumbani mwisho wa mwezi usiku wa manane akiwa kalewa ile mbaya. Ile kufika tu mlangoni kakutana na mkewe akiwa amefura kwa hasira na kubandikwa swali, "Uko wapi mshahara?" Jamaa akainua uso kwa upoole akamjibu, "Nimetumia zote kununua kitu cha hapa nyumbani." Mke akahoji, "Kitu gani hicho na mbona mikononi hujabeba kitu?" Jamaa akajibu, "Nimetumia kuzungusha raundi kumi za pombe baa!" Pata picha kilichotokea...

No comments:
Post a Comment