Saturday, May 5, 2012

ABAKWA NA MUME WAKE SIKU YA NDOA YAO...

Mume amefikishwa mahakamani akidaiwa kumbaka mkewe siku ya harusi yao.
Mwanamke ambaye anakadiriwa kuwa kwenye miaka 20 hivi, ameieleza Mahakama Kuu ya Exeter alikuwa amelewa sana baada ya kurejea kutoka kwenye sherehe za jioni kufuatia harusi yao ambapo alimweleza mumewe kuwa hataki kufanya tendo la ndoa.
Hatahivyo, mumewe alidharau ombi hilo na kumlazimisha kinyume cha matakwa yake, mahakama hiyo ilielezwa.
Mume huyo anashitakiwa pia kwa kumbaka tena mara nne katika miaka miwili ya ndoa yao na mwishowe akaamua kushitaki polisi baada ya kushambuliwa mara mbili ndani ya siku mbili.
Mume huyo amekana mashitaka matano ya kubaka likiwamo lile la siku yao sherehe ya harusi.
Mwendesha mashitaka Richard Crabb alisema tabia ya mume huyo kwa mkewe ilibadilika baada ya harusi na akaendeleza hisia za mfumo dume akimwambia 'wewe ni mke wangu, inaruhusiwa' wakati mkewe alipolalamika kuhusu mashambulio yake.
Mume huyo pia anashitakiwa kwa kumbaka wakati akiwa mjamzito wa kukaribia kujifungua, wakati akiwa bado ana nyuzi baada ya kujifungua mtoto kwa oparesheni na katika matukio mawili baadaye.
Mke amekanusha madai kuwa mashitaka hayo ni njama za kutaka waachane ama kumtia mumewe matatizoni.
Alisema: "Nilikuwa namwogopa. Nilijua hasira aliyokuwa nayo. Nilihofia angewachukua watoto wangu. Hawa ndio uhai wangu.
"Najua haipendezi kusikia, lakini hivi ndivyo ilivyokuwa.
"Nilimpenda kupita maelezo lakini sitaki kuishi kama hivyo tena.
"Usiku wa harusi yetu nakumbuka kusema hapana ni nilisema hivyo kwa sababu nimeolewa naye, nilikuwa na haki ya kusema hapana.
"Nakumbuka kusema vile na kupitiwa na usingizi na mara nikamkuta juu yangu akifanya tendo la ndoa na mimi. Sikutaka kufanya wakati huo. Ndio maana nikasema hapana."
Kesi hiyo bado inaendelea.

No comments: