Saturday, May 5, 2012

AOKOLEWA NA BOTI YAKE BARABARANI...

Kwa zaidi ya mara milioni, nyota wa kipindi cha 'Swamp People', maisha yake yamekuwa yakinusurika kupitia boti yake na hata wakati huu pia, lakini sasa imetokea kwenye Barabara Kuu ya Arkansas.
Joe LaFont na mtoto wake wa kufikia, Tommy Chauvin walikaribia kufa hivi karibu katika ajali iliyohusisha magari matano jirani na mpaka wa Arkansas na Louisiana baada ya lori la mizigo kuligonga kwa nyuma gari walimokuwa.
Kwa mujibu wa LaFont, lori hilo liligonga boti waliyokuwa wakiikokota nyuma ya gari lao, na hiyo ndio sababu amesalimika.
LaFont amesema, wakati lori lilipogonga boti, lilibadili uelekeo badala ya kuwafuata na kuwagonga moja kwa moja.
Aliendelea kusema, "Kama si boti, ningekuwa nimekufa. Ilikuwa kama kishindo cha bomu limelipuka."
Aliongeza kuwa gari lake aina ya F-150 pamoja na tela lake la kukokota mizigo vimeharibiwa kabisa.
LaFonte hakupata majeraha yoyote makubwa japo amesema kuwa amekuwa akisikia maumivu kwenye mabega na shingoni tangu alipopata ajali hiyo hivyo anatarajia kumuona daktari kwa matibabu.
Amesema kwamba hana mpango wowote wa kufungua mashitaka.

No comments: