Akiwa na uso usio na vipodozi na nywele zilizokatwa na kufunikwa na mtandio, huwezi kumtofautisha na masista wenzake wa shirika la Benedictine.
Sista John Mary amejiunga na imani ya milele akiwa na masista wenzake 36 wanaofuata imani ya Mtakatifu Benedict katika shamba lililotengwa lenye ukubwa wa ekari 400.
Ni maisha aliyoitwa kiroho lakini ilikuwa vigumu kwa mrembo huyo mwenye miaka 44 kujiunga nayo wakati alipokuwa akifanya kazi kwenye Makao Makuu ya Chama cha Conservative - akiwa na rafiki yake wa kiume David Cameron.
Laura alianza urafiki na Cameron kuanzia mwaka 1990 hadi mwishoni mwa mwaka 1991, na wakati akifanya kazi Ofisi Kuu ya Conservative, aliendelea hadi kuwa Katibu Muhstasi wa Waziri Mkuu wa wakati huo John Major.
Kisha maisha yao yakachukua mwelekeo mwingine. Cameron alichaguliwa mchepuo wa mambo ya siasa, wakati Laura aliachana na siasa na kwenda kusomea Shule ya Biashara ya Wharton mjini Philadelphia.
Akaja kuwa Mtendaji Mkuu mjini Manhattan kwenye kampuni ya Ogilvy & Mather, wakala wa matangazo wadhamini wa tamthiliya ya Mad Men, lakini mashinikizo ya kimaisha na matatizo binafsi aliyokuwanayo vikamwelemea na kujikuta akiacha kazi.
Hapo Laura akajiingiza kwenye ulimwengu wa ulevi wa kupindukia kabla ya kukutana na wokovu wa Mungu kwenye parokia moja iliyoko vilima vya Connecticut, umbali wa masaa matatu kufika Jiji la New York.
"Nilifikiri maisha yangu yatafanikiwa kwa njia za kawaida za kukutana na mtu, kuolewa, kuwa na watoto, lakini hiyo haikuwa njia ambayo Mungu aliniongoza," amesema Sista John Mary kwenye kipindi kimoja akielezea maisha yake.
Lakini anakiri kwamba maisha yake wakati huo hayakumpa chochote sana sana upweke tu!
Anasema: "Najihisi nilijaribu vitu vingi maishani ambavyo vingekupa furaha. Safari hiyo iniishia kuangukia kwenye ulevi na matumizi ya dawa za kulevya."
Inasemekana kuporomoka kwake maishani kulianza muda mfupi baada ya kuachana na aliyekuja kuwa Waziri Mkuu baadaye.
Mwaka 2007 Cameron, mwenzake wa zamani kwenye makao makuu ya Conservative alimpa Laura 'ruhusa ya Mapumziko maalumu' kujiweka sawa kutokana na machungu ya kuachana.
Pengine kutokana na kuvunja mahusiano na Laura, Cameron anaweza kuamua kutafuta wanawake wengine nje ya ulingo wa siasa.
Baadaye Laura alianza mahusiano na mwanahistoria Andrew Roberts, mmoja wa marafiki wa Cameron.
Lakini mwaka 2008 alijikuta akiandamwa na matatizo ya udhalilishwaji na kuweka wazi kwamba ameamua kuwa Sista. Anakumbushia: "Nakumbuka nilipokuwa nikimwambia mama yangu, "Naenda kujiunga na parokia," na kusema "Ndio, naweza kuona dunia hii haina tena tafsiri bayana kwako." Nilitazama sehemu hii na kuona wanawake wenye kile nilichokitaka.
"Unafanya uamuzi hapa kukabidhi maisha yako kwa Mungu."
Laura anaonekana kufurahia maisha yake hapa kwa moyo wake wote. Filamu inaonesha taratibu zote alizopitia kuweza kujiunga na usista.
Anaonekana akiwa amevalia nadhifu kwa furaha akiwaruhusu masista kukata nywele zake ndefu za kirembo.
Kisha ushungi unazungushwa kichwani mwake kabla ya kuweka nadhiri kwa jina lake jipya.
"Hii ni sehemu pekee ninayoweza kujisikia nipo - sababu hapa ndipo nilipotakiwa kuwa," anasema.
"Anaonekana katika sala, akisali kwa hisia.
"Hakika anawajibika kabisa kwa kanisa," kimesema chanzo cha habari kilichokutana na Laura kwenye misa ambayo waumini walialikwa.
"Mama na dada yake walihudhuria misa. Masista walisali Kilatini. Ilipendeza mno."

No comments:
Post a Comment