Joe Jackson, baba wa mfalme wa muziki wa Pop duniani, Hayati Michael Jackson 'Wacko Jacko' amefunga rasmi fremu yake iliyoko kwenye duka kubwa la Maonesho ya Mitindo mjini Las Vegas.
Kwa mujibu wa mshirika wake wa kuuza pafyumu Julian Rouas Paris ameeleza, "imefungwa sababu maofisa wa duka hilo wamewashusha thamani kwa kuwapa sehemu mbaya kibiashara na kuwatoza kodi kubwa zaidi.
Lakini katika kuonesha kutobabaishwa na yaliyotokea, Baba huyo anayeuza pafyumu za 'Jackson' amefungua fremu mpya mtaani hapo maili saba tu kutoka hapo kwenye duka jingine kubwa la Town Square.
Imeelezwa Joe amependezwa sana na fremu mpya aliyoipata akisema kuwa ina nafasi kubwa na ni jirani zaidi na duka maarufu la pizza California la SCORE.
Hadi sasa hakuna taarifa zozote kutoka kwa wamiliki wa Duka la Maonesho ya Mitindo.

No comments:
Post a Comment