Wednesday, May 2, 2012

CHEKA TARATIBU...

Mzee mmoja mpenda pesa alikuwa kwenye matembezi ya jioni huku kamshika mwanae mkono. Kwa bahati mbaya gari lililokuwa nyuma yao likaacha njia na kumgonga mwanae ambaye alifariki papo hapo. Katika msiba, mzee huyo kwa jinsi alivyokuwa hana utani na pesa akashikilia mwenyewe daftari la michango. Ilipofika jioni si akaanza kuhesabu pesa zilizochangwa. Duh, ikafika Shilingi milioni nane! Yule mzee akiwa amepagawa akaropoka kwa sauti, "Kafa mtoto hata hajulikani zimepatikana hizi, je nikifa mimi si itakuwa balaa!" Watu wote msibani tukabaki tumepigwa butwaa...

No comments: