Wednesday, April 25, 2012

WANASWA WAKIWA WAMETEGA MITEGO HATARI...

PICHA KUBWA: Mitego ya aina mbalimbali mara baada ya kugundulika.
PICHA NDOGO: Benjamin (kushoto) na Kai.

Wanaume wawili wamekamatwa kwa kutengeneza na kutega mitego hatari kwenye eneo la Utah.
Polisi wamewataja Benjamin Steven Rutkowski mwenye miaka 19 na Kai Matthew Christensen miaka 21 wa Provo, wamekiri kutega waya uliofungiwa mpira mkubwa wenye kilo 20 ambao ukifyatuliwa unampiga mtu kichwani ama mtego wa watembea kwa miguu ambapo waya umefungwa kwenye kifundo kilichofungwa kwa kamba na miti iliyochongwa yenye ncha kali mithili ya mishale.
Mitego hiyo iligunduliwa na askari jeshi mwenye mafunzo ya ukaguzi wa ardhini kando ya Big Strings mjini Provo Canyon Jumamosi iliyopita kabla haijaleta madhara yoyote.
Taarifa zilisema kwamba Ofisa Misitu James Schoeffer alikuwa katika doria yake ya kawaida kwenye South Folk Canyon ndipo alipogundua mtego nje ya jengo linalotumiwa na familia linalojulikana kama Ngome.
Mitego hiyo hatari ilitengenezwa mahususi kujifyatua na kumdhuru yeyote aingiaye kwenye makazi hayo.
Mara unapoteguka, mtego huo unaachia kifundo kilichofungwa miti yenye ncha kali iliyofungwa na kamba kwenye mwamba ikining'ingia kutoka kwenye mti.
Katika njia ya pili ya kuingilia kwenye ngome hiyo, mtego mwingine umewekwa maalumu kumfanya mtu kuangukia kwenye miti yenye ncha kali iliyofunikwa na rundo la takataka, wachunguzi wameeleza.
Polisi walisema kuwa wameweza kugundua hilo kupitia mfululizo wa mawasiliano kwenye mtandano wa Facebook baada ya kuongea na familia zilizo karibu na watu hao.
Rutkowski na Christensen wamefunguliwa mashitaka ya kumiliki vitu hatari.
Polisi wamesema wangeweza kushitakiwa mashitaka makubwa zaidi endapo mitego hiyo ingetumika.
Haikuweza kufahamika mara moja nini kiliwasukuma watu hao kuweka vitu vyote hivyo.
Walisema, hakuna dalili zozote kama watuhumiwa hao kama alikuwa na nia ya kuficha chochote, na inaonekana kama walikuwa wakifanya masihara.
Msemaji wa Huduma za Misitu, Sajenti Spencer Cannon alisema: "Tuna imani watakuwa wamejifunza kitu kutokana na hili.
"Nia yetu haikuwa kumfanya mtu akamatwe. Nia yetu ni kumrekebisha mtu tabia na kwamba hii itawasaidia kama watapelekwa jela, hicho ndicho tunachotaka."

No comments: