Polisi wanamsaka nyota wa zamani wa mpira wa kikapu na filamu, Dennis Rodman usiku na mchana, na kwa taarifa za hivi karibuni inasemekana wanakaribia kumnasa baada ya kushindwa kulipia fedha za matunzo ya mtoto.
Rodman anadaiwa Dola za Marekani 179,000 kwa ajili ya kusaidia matunzo ya mtoto. Na pengine tatizo kubwa kwake ni kwamba aliahidi mjini Florida, ambako kuna rekodi ya kufungwa mababa wakorofi.
Baada ya polisi kumtia mikononi Rodman, anaweza tu kutoka dhamana ya Dola za Marekani 4,949.95 ama akaendelea kusota jela.
Pamoja na hayo, Rodman anatafutwa kwa sababu ya kushindwa kutokea katika shauri la kushindwa kutimiza mahitaji ya mtoto wake wa mwisho.
Wanasheria wa siku nyingi wa Rodman, Bradford Cohen na Vanessa Prieto wamesema watampeleka Rodman mahakamani mapema asubuhi 'kurekebisha tatizo hilo'. Wanasheria wamesema Rodman alikuwa hajapata barua ya kuitwa mahakamani, hivyo alikuwa hafahamu chochote kuhusu shauri hilo. Kuhusu kutochangia matunzo ya mtoto walisema wanangoja kusikia watakachosema wanasheria.
Kitu kingine cha mwisho. Kuna madai mengine yanayohusiana na fedha za matunzo ya mtoto yanamuandama Rodman. Anadaiwa zaidi ya Dola za Marekani 800,000 kwa ajili ya matunzo ya mtoto kutoka kwa aliyekuwa mkewe, Michelle Rodman. Dennis ameweka bayana kwamba hana uwezo wa kulipa.

2 comments:
Hi just wanted to say that I like your article very much. Please keep up the good posts Thanks a ton! and Have a good day
You have some genuinely beneficial information composed here. Good job and keep posting good stuff.
HTTP://www.CoolMobilePhone.net
Post a Comment