Ombi la yule babu muuaji Charles Manson, kuomba apate msamaha wa wafungwa limetupiliwa mbali na Bodi ya Parole.
Shauri hilo lilikuwa likisikilizwa kwenye gereza la Corcoran, ambako Manson ambaye alitiwa hatiani kwa mauaji ya watu saba mwaka 1969, akiwamo Sharon Tate, kabla ya hapo alishakataliwa maombi yake ya msamaha mara 11.
Sasa, akiwa na umri wa miaka 77 hii ilikuwa nafasi yake ya mwisho kujaribu kuachiwa, na kesi yake haitoweza tena kusikilizwa hadi baada ya miaka 15 hivyo kufanya aendelee kusota 'lupango' mpaka atakapotimiza miaka 92.
Mfuasi mmoja tu wa Manson, Steve Grogan ndiye amefanikiwa kupata msamaha wa Parole ambaye aliachiwa huru mwaka 1985 kwa kufanya shughuli za kijamii na tabia yake nzuri.
Kama itakumbukwa, Manson alihukumiwa kifo mwaka 1972 lakini hukumu hiyo ikabadilishwa na kuwa kifungo baada hukumu ya kifo California kutangazwa rasmi ni kinyume cha katiba.

No comments:
Post a Comment