JALADA LA UCHUNGUZI WA KIFO CHA WHITNEY LAFUNGWA RASMI...

Whitney Houston amekufa kama ajali ya kawaida baada ya kujizidishia dozi ya dawa za kulevya aina ya Cocaine na hakuna mtu yeyote aliyeshiriki kumuua, Idara ya Polisi ya Beverly Hills kimesema wakati wa kufunga jalada la uchunguzi wa kifo cha mwimbaji huyo.
Idara hiyo imekuwa ikichunguza kifo cha Whitney kwa miezi miwili sasa, tangu Februari 11.
Kama tulivyoripoti, Polisi hawaamini kuna mtu yeyote aliyeondoa dawa za kulevya kwenye chumba cha hoteli sababu tumekuta vifaa na dawa hizo ndani ya chumba cha Whitney katika Hoteli ya Beverly Hilton mjini Beverly Hills.
Cocaine zimechangia kwa kiasi kikubwa kifo cha mwimbaji huyo, alisema Mkemia Mkuu wa Los Angeles.

No comments: