CHEKA TARATIBU...


Usiku mmoja mlevi kaingia baa moja maeneo ya Sinza Kamanyola na kutangaza ofa ya bia kwa wote waliokuwamo ndani pamoja na mhudumu. Mhudumu akafuata maagizo ya yule mlevi kwa kuwagawia watu wote bia bure kisha akampelekea yule mlevi bili ya Shilingi laki sita. Yule mlevi akamjibu kwa kifupi, "Sina pesa!" Kwa hasira mhudumu akamtandika mlevi ngumi za maana na kumtupia nje. Kesho yake mlevi yule yule akaja tena na sera zilezile, huku akidhani ameshika adabu na kujirekebisha kutokana na kichapo cha jana yake, mhudumu akawapa watu wote bia bure. Kama jana yake, mlevi akadai tena hana pesa. Wacha bwana, akala mkong'oto kushinda ule wa jana yake na kutupwa mtaroni kando ya barabara ya Shekilango. Siku iliyofuata mlevi yule akatinga tena baa ileile na kusema, "Wape bia watu woote humu ndani kasoro wewe mhudumu bili kwangu." Mhudumu akahoji kulikoni kanyimwa bia? Ndipo mlevi akajibu kwa kujiamini, "We ukinywa bwana mwishoni unakuwa mgomvi sana, unanipiga." Duh, ama kweli ulevi noma...

No comments: