MTOTO WA MIAKA MINNE AKABANA KOO NA MAPROFESA KWA UELEWA...

Albert Einstein (kushoto) na Profesa Stephen Hawking ambao wote wamemzidi alama moja Heidi. Kulia ni Carol Vorderman ambaye ana alama 154 tu.
Mtoto wa miaka minne amefanikiwa kujiunga na Shule ya Chekechea ya Mtandao wa Mensa kwa kuzoa alama za juu kwenye Maswali ya Uelewa (IQ) na kuwakaribia Stephen Hawking na Albert Einstein.
Mtoto huyo 'Kichwa', Heidi Hankins ambaye bado hajaanza shule alipewa jaribio hilo la kupima uelewa wake baada ya walimu wa shule hiyo kugundua kwamba ana akili zilizopitiliza kiasi cha kuwapa kazi ya kuumiza vichwa zaidi kusaka vitu mbalimbali vya kumpima.
Kijana huyo wa kipekee aliwavutia watahini kwa alama zake 159 alizopata. Wastani wa alama kwa wenye umri mkubwa ni 100 na wale wenye 'kipaji' binafsi ni 130.
Ameweza kumshinda Mwanamahesabu wa runinga, Carol Vorderman (alama 154) ambaye pia mjumbe wa shule hiyo na nyuma kidogo ya Mwanasayansi Mashuhuri Stephen Hawking na Mwanafizikia mkongwe Albert Einstein ambao kwa pamoja wamepata alama 160.
Heidi ambaye tayari anaweza kujumlisha, kutoa, kuchora maumbo na kuandika sentensi, aliweza kusoma kitabu cha mtoto wa miaka saba akiwa na miaka miwili tu.
Jaribio alilofanya, liliandaliwa maalumu kwa mtoto wa rika lake na lilihusisha mchanganyiko wa kutanzua mafumbo na michezo ya kupanga maneno.
Baba wa Heidi, Matthew anayetoka Winchester, Hants, anamatumaini ya kusubiri kwanza mwaka wa masomo ili kuhakikisha amejaribiwa kikamilifu.
Mwalimu huyo wa Afya ya Jamii kutoka Chuo Kikuu cha Southampton mwenye miaka 46 aliongeza: "Mara zote tumekuwa tukiamini Heidi ana akili sana sababu amejua kusoma mapema.
"Nimechanganyikiwa kutokana na uelewa wake na matokeo yamepita kiwango. Nilimnunulia seti nzima ya vitabu vya kusoma vya Oxford akiwa na miaka miwili na alimaliza kusoma seti nzima ya vitabu 30 kwa saa moja.
"Ni kitu ambacho ungetarajia kufanywa na mtoto wa miaka saba.
"Alikuwa akipiga kelele bila mpangilio akijaribu kuongea tangu alipozaliwa na alipotimiza mwaka mmoja akanyoosha maneno vizuri. Sasa ni bora zaidi.
"Alikuwa akiongea sentensi iliyokamilika muda mfupi tu alipoanza kuongea na kisha akaanza kujifunza mwenyewe kusoma kwa kutumia kompyuta akiwa na miezi 18.
"Tuligundua jinsi alivyotumia mausi na kuchezesha na kubofya vitufe vya kukubali ama kukataa.
"Pia aliweza kuchora malkia na wanyama akiwa na miezi 14, ambapo watoto wa rika lake wakiishia kuchora maduara yasiyoeleweka na watu kama viazi."
"Kwa mtazamo mwingine ni kijana wa kawaida anayependa kucheza na watoto wenzake.
"Ni mapema mno kubashiri uelewa wake huo wa ajabu utamfikisha wapi, lakini nadhani amerithi kutoka kwa mama yake ambaye ana kipaji cha uchoraji."
"Hakika tunasikia fahari kuwa naye."

No comments: