Thursday, April 19, 2012

CHEKA TARATIBU...

Kibabu na kibibi vinapata ajali mbaya sana ya gari na kufariki wakati vikiwa njiani kufuatilia majibu ya vipimo vyao hospitalini. Kwa bahati nzuri vyote vikaenda peponi na kupokelewa na Mtakatifu Petro ambaye aliwatembeza sehemu mbalimbali huko na kisha kuwakaribisha kwenye chumba chenye kila kitu unachofikiria. Baada ya kuwakabidhi chumba hicho chenye raha zote, Petro akaaga na kuwaacha wawili hao. Ndipo kile kibabu kikaanza gubu, "Wewe ni mwanamke mjinga sana. Umeona raha zote hizi? Hapa tungekuwa tumekuja miaka ishirini iliyopita kama si ujinga wako wa kukimbilia haraka hospitali kila tunapoumwa." Duh, kibabu kimepinda kweli...

No comments: