Thursday, April 19, 2012

HULK HOGANA AUZA JUMBA LAKE KWA BEI YA HASARA...

Kwa lugha nyingine hapa Bongo tunaweza kusema amefulia ama ukipenda ukamwita anafanya nyodo!
Lakini ukweli ni kwamba mwanamieleka mkongwe Hulk Hogan hatimaye ameuza jumba lake lenye eneo la ukubwa wa futi za mraba 17,000 kwa Dola za Marekani milioni 6.2, ikiwa ni chini kwa zaidi ya Dola za Marekani milioni 18 kutoka kwenye bei aliyotangaza ya awali.
Hogan, ambaye jina lake halisi ni Terry Bollea, alinunua ardhi hiyo pamoja na aliyekuwa mkewe, Linda mwaka 1992 kwa Dola za Marekani milioni 2 na kujenga jumba mwaka 1996.
Aliliweka sokoni mara tu Linda alipofungua kesi ya kudai talaka na gharama za kuendesha kesi hiyo zilimfyonza kiasi kikubwa cha pesa za mwanamieleka huyo.
Wakati wa mfululizo wa vipindi cvya televisheni vya 'Hogan Knows Best', alipigwa picha akiwa kwenye nyumba ya kawaida tu.
Miaka mitano, Hogan alitangaza kuuza jumba hilo kwa Dola za Marekani milioni 25, limeripoti gazeti la Tampa Bay Times.
Kufuatia kuyumba kwa soko la nyumba, mwanamieleka huyo nyota kwa mshangao akashusha hadi bei chini kabisa.
Kulingana na taarifa za mtandao wa celebritynetworth.com, Hogan bado ana utajiri unaofikia Dola za Marekani milioni 30, sababu bado anapokea gawio kutoka nembo katika yake ya Hulk Hogan.
Pia Hogan amewekeza kwenye mashamba na biashara nyinginezo.

No comments: