Tuesday, April 17, 2012

CHEKA TARATIBU...

Jamaa mmoja kipofu akitokea kilabuni kuelekea kwake usiku mara akatumbukia kwenye shimo na kupoteza fahamu. Mara tu fahamu zilipomrudia, akaanza kupiga kelele za kuomba msaada. Kwa bahati kijana aliyekuwa akipita akasikia kelele zile na kuelekea liliko lile shimo. Baada ya juhudi kadhaa za kumtoa kushindikana ndipo kijana akapata wazo la kutafuta kamba. Akamwambia yule mzee ashikilie ile kamba huku yeye akivuta. Mzee akajibu, "Mwanangu, sina mikono." Kijana akajibu, "Ooh pole sana! Basi ng'ata kamba kwa nguvu." Mzee akafanya kama alivyoagizwa na zoezi kuelekea kufanikiwa. Sasa wakati alipochomoza juu ya shimo huku kijana akitabasamu kwa kufanikiwa, yule mzee si akataka kumshukuru kijana kwa msaada wake. Ile kufungua tu mdomo akabwagika tena shimoni kama kiroba na kupoteza fahamu. Duh, kijana kuona vile akatoka nduki...

No comments: