Tuesday, April 17, 2012

MABAKI YA VITU YAKUTWA KWENYE MELI YA TITANIC...

Picha zilizotolewa hivi karibuni zimeonesha mabaki ya nguo za waathirika waliokufa wa ajali ya meli ya Titanic miaka 100 baada ya meli hiyo ya New York kuzama huko Atlantic Kaskazini, zikiwa kwenye sakafu ya mabaki ya meli hiyo.
Picha ya mwaka 2004, iliyooneshwa hadharani kwa mara ya kwanza wiki hii ambayo haijachongwa ili kuweka uhalisia wa janga lenyewe, imeonesha koti na viatu yakiwa kwenye matope katika eneo ilipozama meli hiyo.
Tukio hilo limekuja wakati abiria wa meli ya kitalii waliokuwa wakifuatilia maeneo ilimopita meli hiyo iliyoangamiza maelfu ya watu ya RMS Titanic, walipokuwa wakiadhimisha misa ya kumbukumbu kwenye eneo sahihi ilipozama meli hiyo ikiwa safariki karne iliyopita.
"Hivi si viatu vilivyoanguka kutoka kwenye begi la mtu pembeni ya mwenzake," alisema James Delgado, Mkurugenzi wa Makumbusho ya Meli katika Mamlaka ya Bahari na Mazingira yake.
"Jinsi vilivyo hapa vinathibitisha ni mahali ambako mtu mmoja alikuja kupumzika," alisema.
Picha, sambamba na nyingine mbili inaonesha jozi za viatu zikiwa jirani ya zingine, ilipigwa wakati wa zoezi ya utafiti ulioongozwa na NOAA na Mtafiti mashuhuri wa Titanic Robert Ballard mwaka 2004.
Zilichapishwa kwenye kitabu cha Ballard wakati wa utafiti huo. Delgado alisema kuwa moja inayoonesha koti na mabuti, imechingwa kuonesha mabuti pekee.
Gazeti la New York Times liliripoti kwa mara ya kwanza kuhusu picha hizo katika toleo la Jumamosi.
Mtengeneza filamu James Cameron, ambaye alitembelea mabaki ya meli hiyo mara 33, alisema hakukuwa na mabaki yeyote ya binadamu wakati wa utafiti wa kina wa Titanic.
"Tumeona viatu. Tumeona jozi za viatu, vinavyothibitisha kabisa kuwa kulikuwa na mwili pale. Lakini hatukuona kabisa mabaki yoyote ya binadamu," alisema Cameron.
Kwake Delgado, ambaye alikuwa mwanasayansi mkuu wa utafiti wa mwaka 2010 ambao ulichora ramani ya eneo lote la ajali, alitofautiana na Cameron katika maoni yake.
"Kama mtafiti wa mambo ya kale ningeweza kusema vyote hivyo ni mabaki ya binadamu," alisema, akirejea moja kwa moja picha za koti na mabuti.
"Kuzikwa kwa staili ile ni sawa kabisa kwa vitu hivyo kutambulika kama mabaki ya mtu husika."
Alieleza kwenye baruapepe kwamba picha 'zinasema nguvu ya janga na ugumu wa eneo la tukio maili mbili na nusu chini' na kufanya makumbusho ya chini ya bahari.'
"Ni ni fursa ya kuona thamani ya mwanadamu katika tukio lile, na ukweli kwamba katika sehemu hii maalumu chini kabisa ya bahari, ushahidi wa thamani ya mwanadamu, katika hali ya chombo kilichoangamia, mizigo iliyosambaratika, vifaa na mambo mengine, na ushahidi hafifu lakini ambao haukukosewa ni mahali watu walipokuja kufia, bado pamekuwepo," alisema.
Alisema pia picha hizo ni ushahidi kuwa jamii inaweza kufanya kazi kubwa zaidi kulinda eneo hilo la ajali.
Kumekuwa na mapambano makubwa sana kuilinda Titanic tangu ilipogunduliwa tena na Ballard mwaka 1985, ikianzia na sheria iliyopitishwa na chama cha Congress ikikusudia kuweka makubaliano ya kimataifa ya kuyabadili mabaki ya meli hiyo kuwa kumbukumbu ya kimataifa ya usafiri wa majini.
Dk. Robert Ballard, ambaye aligundua mabaki ya meli hiyo mwaka 1985, yupo mjini Belfast kwa ajili ya maadhimisho ya kumbukumbu ya Titanic yaliyofanyika jana. Juzi alitoa mada kuhusu kumbukumbu hiyo.
Misa ya mazishi kukumbukia tukio hilo pia itafanyika kwenye Kanisa la Mtakatifu Anna, mjini Belfast.
Hii ni moja ya tiketi zilizotumika wakati wa safari ya meli ya Titanic miaka 100 iliyopita ambayo hata hivyo haikumaliza safari yake na kuzama ambapo iliua maelfu ya abiria na wafanyakazi wa meli hiyo.

No comments: