Monday, April 23, 2012

ALIYEZAA NA BINTI YAKE WATOTO WATATU AFUNGWA JELA MIAKA MITANO...

Jengo la Mahakama Kuu ya Caernarfon iliposikilizwa kesi hiyo.
Mwanaume mmoja ambaye ameishi na binti yake kama 'mume na mke' mpaka kuzaa naye watoto watatu, amefungwa jela jana.
Mwanaume huyo mwenye miaka 47 kutoka eneo la Conwy mjini North Wales alielezwa na Jaji Merfyn Hughes QC kwamba msichana huyo 'alikuwa chini ya dhamana yake kwa asilimia zote.'
"Alikuwa ni binti yako wakati ulipoanza kumdhalilisha," aliongeza.
Mwanaume huyo baba wa watoto watatu pamoja na binti yake huyo, alihukumiwa kifungo cha miaka mitano na miezi kumi jela na kuorodheshwa moja kwa moja kama mbakaji.
"Umekuwa mlezi mwenye dhamana ya maisha yake hadi ulipoanza udhalilishaji huu. Unaweza kufanya hivi kwa msichana mwingine tena kama yeye."
Mwanaume huyo, ambaye hakutajwa jina kulinda utambulisho wa binti, alikiri kuwa na mahusiano ya kimapenzi na binti yake wakati huo binti akiwa mwanzoni mwa umri wa miaka 20.
Alifungwa miaka mitano na miezi kumi na kuorodheshwa moja kwa moja kama mbakaji.
Jaji Hughes alisema katika Mahakama Kuu ya Caernarfon: "Kuna mambo ya kuzingatia na yenye tija kuhusu vipimo vya vimelea katika matukio yote matatu."
Amri ya kuzuia matukio ya kujamiiana ilitolewa ambayo inazuia kukaribiana na mwanamke na watoto ila tu kwa idhini ya mamlaka zinazohusika na huduma za jamii.
Mwanaume huyo amepigwa marufuku mahusiano yoyote au kuishi na mtu mzima yeyote mwenye watoto bila kuzitaarifu mamlaka zinazohusika na huduma za jamii.
Mwendesha mashitaka Kate Meredith-Jones alisema binti huyo alikuwa na miaka 15 wakati baba yake alipomweleza kuwa ameshindwa kuzuia hisia zake kimapenzi kwake.
"Alifanywa ajihisi wa kipekee," alisema mwendesha mashitaka huyo. "Alieleza kila kitu kuhusu alivyomnywesha wiski ambayo kwa kawaida huwa hanywi."
Mwanaume huyo alimbusu binti yake lakini alisukumwa katika tukio hili akisema: "Hapana, huwezi - wewe ni baba yangu."
"Alikuwa ni binti mdogo sana wakati ulipoanza kumdhalilisha. Ulikuwa na dhamana ya kulinda maisha yake milele. Unaweza kusababisha matatizo kwa mwingine kama binti huyu."
Lakini siku iliyofuatia walifanya tena ngono na karibu kila siku baadaye iliendelea hivyo.
Binti huyo aliieleza polisi kwamba alikuwa 'mshiriki aliyeridhia hivyo.'
Mwendesha Mashitaka aliongeza: "Waliishi kama mume na mke, wakichangia kitanda."
Baada ya kujifungua mtoto wa kwanza, mamlaka za huduma za jamii ziliingilia kati lakini binti huyo na baba yake walidai ni mtu mwingine ndiye baba wa mtoto huyo.
Jaji alisema familia hiyo ilikaa kimya na kuhakikisha siri haitoki nje baada ya mtoto wa pili kuzaliwa.
Mwanaume huyo alijua fika mamlaka zitafuatilia kujua kinachoendelea kwenye nyumba hiyo.
Ukweli ukajidhihiri baada ya binti huyo kubeba mimba tena kwa mara ya tatu.
Msemaji wa upande wa utetezi alisema: "Alikiri hakuna anachoweza kusema zaidi ya kuomba msamaha kwa alichofanya na yote yaliyotokea."
Aliongeza: "Binti huyo anataka mwanaume huyo aruhusiwe kurejea nyumbani kwa familia yake. Ni hali ya kuchanganya sana."

No comments: