Arnold Schwarzenegger amekamatwa kwa kosa la kuendesha kizembe kwa mwendo kasi gari lake kwenye mitaa ya Beverly Hills juzi.
Nyota huyo wa filamu ya The Terminator alikuwa akitimua mbio na gari lake aina ya Mercedes AMG katika njia ya vumbi kwenye moja ya mitaa ya mji wa Beverly Hills ndipo ghafla aliposimamishwa na askari polisi.
Baada ya mahojiano kwa dakika kadhaa, Arnold alikiri kosa huku akitabasamu na hivyo kutozwa faini ya Dola za Kimarekani 400.
Gavana huyo wa zamani alilipa faini na kuachiwa aendelee na safari yake kwa usalama.
Arnold amewahi kutamba katika filamu nyingi za kibabe ikiwamo ile ya The Expendables.

No comments:
Post a Comment