Monday, April 23, 2012

CHEKA TARATIBU...

Jamaa mmoja kaenda kwenye duka kununua akili ili azitumie kumalizia masomo yake ya uanasheria. Alipoingia akaona vibao mbalimbali vikionesha ubora tofauti tofauti wa akili zinazouzwa dukani humo. Akaanza kumuuliza muuzaji kuhusu gharama zake na mahojiano yalikuwa hivi:
Jamaa: Kilo moja ya akili kwa ajili ya kuwa Injinia nauzaje?
Muuzaji: Shilingi elfu tatu!
Jamaa: Je, akili kwa ajili ya kuwa Daktari?
Muuzaji: Shilingi elfu tano!
Jamaa: Na akili kwa ajili ya kuwa Mwanasheria?
Muuzaji: Shilingi laki mbili!
Jamaa: He! Mbona bei kubwa hivyo braza?
Muuazaji: Ebo! Ungejua inanibidi kuua wanasheria wangapi ili kupata robo kilo tu ya akili usingeshangaa dogo!
Mmmh, kweli kua uyaone...

No comments: