Wednesday, March 14, 2012

YANGA IMENIKUMBUSHA MBAAAAALI...

Video hii inaonesha wachezaji wa Yanga wakimshambulia mwamuzi wa pambano lao la Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC ambapo baada ya wachezaji wake wawili kulimwa kadi nyekundu mapeeema, wakaamua kugeuza Uwanja wa Taifa kuwa ulingo wa masumbwi. Mechi hiyo ambayo Yanga ilichapwa mabao 3-1, imenikumbusha miaka ya 1990 wakati Ligi Daraja la Tatu Dar es Salaam ikiwa na msisimko mkubwa. Wakati huo vitendo vya marefa kudundwa kwa tuhuma za upendeleo vilikuwa havikosekani katika kila mechi hasa baada ya filimbi ya mwisho kupulizwa. Kuna wakati fulani kwenye viwanja vya Biafra, Kinondoni mwamuzi mmoja kadri muda ulivyokuwa ukiyoyoma yeye alikuwa akijisogeza kando ya uwanja jirani na nyumba moja na filimbi ya mwisho alipuliza akiwa anatokomea kwenye geti la nyumba hiyo. Yanga kweli imeandika historia katika karne hii. -Mdau wa Soka

No comments: