Wednesday, March 14, 2012

YANGA YAISASAMBUA LYON, SIMBA YAIZIMA POLISI DODOMA...


Mchezaji wa timu ya African Lyon, Ahmad Manzi akihamisha mpira mbele huku Kenneth Asamoah (kushoto) na Kigi Makasi wa Yanga (kulia) wakijiandaa kumkabili wakati wa mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Yanga ilishinda goli 1-0.
Wakati mabingwa watetezi Yanga wakiisasambua African Lyon bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa, mahasimu wao Simba walifanikiwa kuwapigisha kwata maafande wa Polisi Dodoma katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma. Katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa, Yanga ambayo ilicheza bila wachezaji wake nyota wanne, ilipata bao lake katika dakika ya 43 mfungaji akiwa Kiggi Makassy. Dodoma, bao la Simba liliwekwa kimiani na Patrick Mafisango.

No comments: