OFISI INAPANGISHWA...

Sidhani kama aliyetoa wazo alitaka haya ndio yawe matumizi ya Ofisi hii maeneo ya geti la mwisho Changanyikeni Majumba Ishirini. Ofisi hii pichani ilijengwa kwa ajili ya askari wanaofanya upekuzi kwa magari yote yanayoelekea Changanyikeni lakini badala yake kimetelekezwa na kwa zaidi ya miezi sita sasa kimekuwa hakitumiki. Kwa kifupi tunaweza kusaidia kutangaza tenda ya kukipangisha kwa yeyote anayetaka kuweka biashara yake ama kuishi. Teh, Teh, ni mtazamo tu!!

No comments: